- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Maadhimisho ya Miaka 60 katika Halmashauri ya Shinyanga MC iliadhimishwa kwa Aina yake Kwa Ufunguzi wa Machinjio ya Kisasa pamoja Na Kampeni ya Upandaji Miti ya Matunda na Kivuli
Umuhimu wa Cheti cha Kuzaliwa
Ni utambulisho wa awali kisheria utakaomuwezesha mtoto kupata haki nyingine.
Humsaidia mtoto kuandikishwa shule za msingi na sekondari.
Kuzuia ajira ya watoto na kuwalinda watoto wanaokinzana na sharia.
Kuwawezesha wanafunzi kujiunga na vyuo na elimu ya juu.
Kupata mikopo ya elimu ya juu.
Ni lazima ili kupata ajira katika taasisi za serikali na majenshi ya ulinzi na usalama.
Ni kiambatanisho cha msingi ili kupata kitambulisho cha Taifa katika zoezi linaloendelea nchini.
Husaidia kupata hati ya kusafiria (Passport)
Zoezi la kuwasajili na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa bila malipo watoto wote walio na umri chini ya miaka 5 linaendelea katika kila ofisi za mtendaji wa kata na vituo vya afya vinavyotoa huduma ya mama na mtoto. Katika picha Bi.Evelyne Muuguzi Msaidizi katika kituo cha Afya cha Magereza, kilichopo mtaa wa Ushirika, kata ya Chamaguha, Manispaa ya Shinyanga akimkabidhi mzazi cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili katika daftari la usajili.
Mara baada ya kusajili na kupokea cheti cha kuzaliwa wazazi huelemishwa kuwa cheti kinachotolewa ni halali kwa matumizi yoyote. Na pia cheti hakina ukomo wa matumizi ya mtoto hatalazimika kupata cheti kingine baada ya umri wa miaka 5. Kwa hiyo ni vema cheti kitunzwe mahali salama na kisikunjwe.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa usajili na utoaji wav yeti vya kuzaliwa ni kama ifuatavyo:
Mzazi au mlezi anatakiwa kufika na kadi ya kliniki au tangazo la kuzaliwa mtoto au cheti cha ubatizo wa mtoto.
Mzazi au mlezi afike na taarifa sahihi za jina la mtoto na majina matatu sahihi ya wazazi wa mtoto yaani baba na mama wa mtoto.
Tafadhali angalia utekeleaji wa serikali mtandao katika utoaji wa huduma kwa wananchi
Shinyanga Municipal
Anwani ya Posta: P.O.Box 28,Shinyanga
Simu: 028-2763213
Simu ya Mkononi: 0767042958
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga