- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Baraza la Ushauri la Wazee Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Septemba 20, 2025 limeadhimisha Siku ya Wazee Duniani kwa ngazi ya halmashauri kwa kutoa msaada wenye thamani ya zaidi ya shilingi 300,000 katika Kituo cha Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto.
Katika maadhimisho haya, wazee wanaolelewa kituoni hapo wameishukuru Serikali pamoja na Baraza hilo kwa kuendelea kuthamini na kutambua mchango wao mkubwa walioutoa katika kulipambania taifa na kudumisha maadili ya Kitanzania kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Stephano Tano, amesema msaada huo ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya ngazi ya mkoa yatakayofanyika Septemba 23, 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Naye, Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Shinyanga, Bi. Elizabeth Mweyo, amesema Serikali imeendelea kuthamini mchango wa wazee katika historia ya taifa, na ndiyo maana ilianzisha makazi maalum ya kuwatunza wazee wasiojiweza ili kuhakikisha wanapata huduma muhimu ikiwemo matibabu.
Kwa upande wake Msimamizi wa Kituo cha Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto, Bi. Sophia Kang’ombe, amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1975 na ni miongoni mwa kambi 13 za aina yake nchini ambapo Hadi sasa kituo kina jumla ya wazee 18, wakiwemo wanaume 11 na wanawake 7.
Nao baadhi ya wazee wanaolelewa katika kituo hicho wamesema wameridhishwa na huduma wanazopata, huku wakitoa shukrani kwa Serikali na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa namna inavyowapa kipaumbele, hasa wanapokumbwa na changamoto za kiafya
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga