- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
UTARATIBU WA KUPATA LESENI ZA BIASHARA
Leseni zote za Biashara hutolewa chini ya Sheria ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake yaliyofanyika mwaka 1980. Mwombaji wa leseni ya biashara anapaswa ajaze fomu ya maombi ya leseni TFN 211 fomu_ya_maombi _ya_leseni.pdf.
Leseni za Biashara zimegawanyika katika makundi mawili:
KUNDI A: Leseni hizi hutolewa na Wizara ya viwanda na Biashara ambazo ni;
•Uagizaji wa bidhaa toka nje (Import license)
•Kusafirisha bidhaa nje (Export license)
•Wakala wa mali (Estate Agent)
•Hotel za Kitalii (Tourist Hotel & Lodging)
•Wakala wa kupokea na usafirishaji mizigo (Clearing & Forwarding & Freight forwarders) nk.
KUNDI B: Hizi hutolewa na Halmashauri ya Manispaa/Wilaya/Miji/Jiji husika mfano:
•Wakala wa Bima (Insurance Agent) •Vipuri (Spare parts, Machine Tools) •Maduka ya dawa za binadamu/ Mifugo •Viwanda vidogo (Small scale manufacture and selling) •Uuzaji wa bidhaa Jumla na rejareja (Wholesale & Retail trade) n.k
MASHARTI YA KUOMBA NA KUPEWA LESENI ZA BIASHARA.
i.Mfanyabiashara anapaswa awe na hati ya usajili iwapo anatumia jina la biashara (Certificate of Registration or Incorporation)
ii.Kama ni Kampuni mwombaji awe na “Memorandum /Article of Association” ambazo zinaonyesha kuwa kampuni imeruhusiwa kufanya biashara anayoiomba.
iii.Awe na mahali/ Eneo linalokubalika kwa aina ya biashara anayoiomba naisiwe vibanda vilivyopo kando kando ya barabara.
iv.Mfanyabishara aje na kivuli cha Cheti cha namba ya mlipa kodi (TIN) pamoja na kivuli cha cheti kinachoonyesha kuwa umelipa mapato kwa mujibu wa Sheria (Tax Clearance) ambavyo vyote vinatolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
v.Masharti mengine ya kupata Leseni hutegemea aina ya biashara mtu anayetaka kuanzisha eg. Mgahawa inadidi afuate taratibu zote za afya na kupima wafanyakazi wake.
vi.Hati ya Utaalamu (Professional Certifucates) kwa biashara zote za kitaalam.
MALIPO
Ada ya Leseni inatofautiana kulingana na aina ya Biashara inayofanyika.
Adhabu
Asilimia 39% ya ada ya Leseni ya Biashara itatozwa kwa yeyote ambaye atafanya Biashara bila Leseni au Atakae chelewa kukata au kuhuwisha Leseni yake kwa wakati.
Endapo atachelewa kufanya hivyo zaidi ya mwezi mmoja adhabu inaongezeka kwa asilimia 2% zaidi kila mwezi unaofuata.
LESENI ZA VILEO
Biashara ya vileo inatekelezwa kwa kufuata Sheria ya mwaka 1968, Kifungu 28 (Liquor License Act No. 28 of 1968) na marekebisho ya sheria hiyo yaliyofanywa mwaka 2004.
UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA LESENI.
Maombi yote mapya ya Leeseni za vileo ni lazima yapitishwe na wataalam ambao wameainishwa kwenye Fomu ya maombi (Watendaji/Wenyeviti wa kata husika ambako biashara inafanyika/Inatarajiwa kufanyika,Afisa Afya, na Afisa Biashara.Fomu ya Leseni za Vileo.pdf
Maombi yote yanayorudiwa (Renewal) yawasilishwe moja kwa moja kwa Afisa biashara anayeshughulikia leseni za vileo kwa utekelezaji zaidi.
Leseni za vileo hutolewa kwa vipindi viwili (2) ambapo kipindi cha kwanza huanzia tarehe 1/04 hadi 30/09 na kipindi cha pili huanzia tarehe 1/10 hadi 31/03 mwaka unaofuata.
ADA:
Maombi mapya na yanayorudiwa hulipiwa ada ya Jumla ya Tsh. 40,000 – kwa wale wanaouza pombe katika maeneo yao ya biashara (Retailers On),
Tsh 30,000 kwa wale wenye biashara ya vileo vilivyofungwa kwenye maduka ya rejareja(Retailers off),Tsh 20,000 kwa wale wenye biashara ya vileo vya jumla katika klub ya wanachama (Club/Whole sale)
na ada ya fomu Tsh 2,500/= na kwa wale wanaouza Pombe za Kienyeji hulipia ada ya Tsh. 12,000 (Local Liquor).
Aidha wanaoendesha biashara ya vileo bila kufuata taratibu zilizotajwa hapo juu huchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kupelekwa Mahakamani kulipishwa faini pamoja na penalty au kufungiwa biashara zao.
WAJIBU WA MFANYABIASHARA.
•Kulipia Leseni ya Biashara au Kuhuwisha ni wajibu wa kila mfanya Biashara kulingana na Sheria ya Biashara N0. 25 ya mwaka 1972 ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2004 .
•Ni jukumu la kila mfanyabishara kumiliki leseni katika eneo lake la biashara na kuiweka mahala pa wazi ili kuonekana kwa urahisi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga