- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa kutambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya jamii, imeandaa mafunzo elekezi kwa walimu wa shule za sekondari kwa lengo la kuwajengea uelewa na kuongeza uwezo wao katika utekelezaji wa Mtaala Mpya Ulioboreshwa wa Elimu ya Sekondari.
Mafunzo hayo yamewakutanisha takribani walimu wawakilishi 170 kati ya walimu 496 kutoka shule 22 za sekondari zilizopo ndani ya Manispaa ya Shinyanga, hususan walimu wa masomo ya sayansi, sayansi ya jamii pamoja na elimu ya biashara.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Dedan Rutazika, ameipongeza Idara ya Elimu Sekondari ya Manispaa ya Shinyanga kwa kuendelea kuzingatia mabadiliko ya mitaala ya elimu na kuandaa mafunzo elekezi yanayolenga kuwajengea walimu uelewa na uwezo wa kutekeleza mitaala hiyo ipasavyo.
Kwa upande wake, Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Richard Makoye, amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea walimu uelewa wa namna bora ya kuandaa na kutumia zana za kufundishia na kujifunzia, ili kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi, sayansi ya jamii pamoja na elimu ya biashara kulingana na matakwa ya mtaala mpya.
Nao baadhi ya walimu walioshiriki mafunzo hayo wameishukuru Idara ya Elimu Sekondari kwa kuandaa mafunzo hayo, ambapo wamesema mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza maarifa na uelewa wa mtaala ulioboreshwa, hususan katika masomo ya kidato cha kwanza na pili, hatua itakayochangia kuboresha ufaulu wa wanafunzi na kuwawezesha kufikia ndoto zao za kielimu.
Manispaa ya Shinyanga imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuinua ufaulu wa elimu ya sekondari, ikiongozwa na kaulimbiu yake isemayo “Shinyanga Municipal, Let Us Push Together.”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga