- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Wakili Julius Mtatiro, amewataka wananchi kuacha kukopa mikopo umiza maarufu kausha damu kutokana na athari zake kwa ustawi wa maisha yao na maendeleo ya kiuchumi.
Mhe. Mtatiro ametoa wito huo leo Januari 06, 2026, wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita katika mkutano wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi uliofanyika katika viwanja vya Zimamoto - Nguzonane, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika mkutano huo, Wakili Mtatiro amewasihi wananchi kuachana na mikopo hiyo yenye riba kubwa na badala yake kujikita katika mikopo isiyo na riba ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato yake ya ndani huku akibainisha kuwa mikopo hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kiuchumi bila kuwaumiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze, amesema kuwa katika jitihada za kuwanusuru wananchi dhidi ya mikopo umiza, Halmashauri tayari imeidhinisha zaidi ya shilingi milioni 490 kwa ajili ya vikundi 30 vya kinamama, vijana na watu wenye ulemavu vilivyokidhi vigezo vya kupatiwa mikopo hiyo.
Katika hatua nyingineMwl. Kagunze amewahimiza wananchi kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mikopo hiyo isiyo na riba huku akisisitiza kuwa lengo la Halmashauri ni kukuza uchumi wa wananchi na kuimarisha ustawi wa jamii kwa ujumla.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga