- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
IDARA YA UCHUMI NA MIPANGO
Idaraya Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia na uunganishaji wa shughuli zote za upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo ya Halmashauri, Usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, ukusanyaji wa Takwimu, utayarishaji wa bajeti, pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji katika Manispaa ya Shinyanga. Pia Idara inajishughulisha na uandaaji na kuwasilisha taarifa mbalimbali zinazoandaliwa na Idara zingine zilizopo kwenye Halamshauri na katika Ngazi ya Kata na Vijiji.
Idara hii imegawanyika katika sehemu Kuu tatu (3) kama ifuatavyo:-
Sera na Mipango
Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo.
Takwimu.
SEHEMU YA SERA NA MIPANGO.
Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-
Kuratibu uandaaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD kila mwaka .
Kuratibu na kuandaa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri.
Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo (Project Proposal).
Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka.
Kusimamia uandaaji wa Mpango kazi (Action Plans) na Mtiririko wa fedha (Casha Flow) ya bajeti kila mwaka
Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri.
Kusimamia utayarishaji na uandaaji wa Taarifa za utekelezaji wa Hesabu za Serikali kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)
SEHEMU YA USIMAMIZI, UFUATILIAJI NA TATHMINI YA MIRADI YA MAENDELEO.
Majukumu ya sehemu hii yapo kama ifuatavyo:-
Kufanya ufuatiliaji na Usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Halmashauri kila robo mwaka
Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka
Utasimamia na kuratibu fedha za miradi ya maendeleo kutoka mapato ya ndani ya 40% ya Halmashauri ili kuhakikisha kila mwezi tunatengewa
SEHEMU YA TAKWIMU.
Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-
Kuratibu na kusimamia benki ya Takwimu ya Halmashauri.
Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Social-economic Profile) ya Halmashauri.
Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.
Kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri.
Kukusanya, kuandaa kuchambua na kutoa takwimu na taarifa mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa wadau.
Kutunza na kuimarisha matumizi ya mifumo muhimu ya Takwimu ikiwemo Mifumo ya upangaji na utoaji taarifa (Plan – Rep, LGMD, Rejista za wakazi na BREMIS).
Takwimu za Haraka
Idadi ya Maoteo ya watu kwa Mwaka 2018 Watu = Me 98,289, Ke 103,508 Jumla 201,797
Idadi ya Tarafa - 03
Idadi ya Kata - 17
Idadi ya Mitaa - 55
Idadi ya Vijiji - 17
Idadi ya Vitongoji – 84
Ukubwa wa Eneo ni Km za Mraba 548
Idadi ya Shule za Msingi za Serikali - 48
Idadi ya Shule za Msingi za Binafsi –
Idadi ya Shule za Sekondari za Serikali – 17
Idadi ya Shule za Sekondari za Binafsi –
Bajeti ya Mwaka 2019/2020 – Tsh 28,386,979,090
Mapato ya Ndani kwa Mwaka 2019/2020 Tsh 3,023,228,546
Asilimia 40 ya Mapato ya ndani kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo Tsh 1,196,000,000
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga