- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita amewataka wananchi na wafanyabiashara mkoani Shinyanga kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kulinda afya ili kuendeleza kuyafanya mazingira kuwa bora na salama.
Akizungumza leo, Septemba 20, 2025, katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Usafishaji Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Soko la Matunda Kambarage, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mhe. Mhita ameipongeza Manispaa hiyo kwa kuendelea kushika nafasi za juu kwa miaka kadhaa katika ushindani wa kitaifa wa usafi wa mazingira.
“Manispaa yetu ya Shinyanga imekuwa kinara kwa miaka kadhaa katika suala la usafi wa mazingira. Hii ni ishara kwamba kwetu usafi siyo tukio la msimu, bali ni utamaduni. Nawapongeza wananchi wote chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Manispaa kwa kutetea heshima hii. Hata hivyo, tunapaswa kuongeza jitihada zaidi kuanzia kwenye familia, mitaa, maeneo ya kazi na masoko ili tuendelee kuwa mfano bora kwa taifa.” amesema Mhe. Mhita.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze, Amesema katika kuthamini mazingira ya wafanya biashara, Serikali kupitia mradi wa TACTIC unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, imepanga kubomoa na kujenga upya Soko la Kambarage ili kuboresha mazingira ya wafanyabiashara na kuwapatia miundombinu ya kisasa zaidi.
Maadhimisho ya Siku ya Usafi Duniani 2025 yamebeba kaulimbiu isemayo: “Tunza Mazingira kwa Kuzipa Taka Thamani.”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga