- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wahitimu wa kidato cha nne mwaka 2025 Shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga wameahidi kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa wa kidato cha nne unaotarajiwa kuanza Novemba 10, 2025.
Ahadi hii wameitoa leo Septemba 18, 2025 wakati wa mahafali ya 16 ya kidato cha nne ambapo wamesema kuwa mazingira bora ya kujifunzia na juhudi za walimu wao yamewaandaa ipasavyo kufanikisha ndoto zao za kitaaluma.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Shule ya Sekondari hiyo, Mwl. Hamisa Boniphace, amewashukuru walimu na wazazi kwa mshikamano na ushirikiano wao katika kuhakikisha wanafunzi wanapata malezi na elimu bora.
Kwa upande wake, Mwl. Richard Makoye, ambaye amemwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, amewasihi wazazi kuendelea kuwapatia watoto muda wa kutosha na mazingira tulivu ya kujisomea ili waweze kufanikisha malengo yao.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye ni Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Vijana Tanzania na Mkurugenzi wa Africa Mining Investment Fund Mhe. Magreth Baraka Ezekiel amewahimiza wahitimu hao kuendelea kuzingatia elimu kama nguzo ya mafanikio ya maisha na maendeleo ya taifa.
Ikumbukwe kuwa Shule ya Sekondari Ndala imeendelea kuonyesha mwanga chanya katika elimu ambapo Mwaka 2024 shule hiyo ilishika nafasi ya 3 kati ya shule 21 za serikali katika Manispaa ya Shinyanga kwa jumla ya ufaulu wa asilimia 95, ikilinganishwa na asilimia 90 mwaka 2023.
Mafanikio haya yameongeza matumaini makubwa kwa wanafunzi wa mwaka 2025 kuwa nao watafanya vizuri na kuongeza hadhi ya shule hiyo kitaaluma.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga