- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka watu wenye ulemavu wa kusikia (VIZIWI) kushiriki kikamilifu katika suala la kugombea katika uchaguzi wa serikali za mtaa utakaofanyika Novemba 27, 2024 na kushiriki katika kupiga kura.
Mhe. Macha ameyasema haya leo Jumatano Septemba 25, 2024, katika ufunguzi wa maadhimisho ya kumi na moja (11) ya watu wenywe ulemavu wa kusikia(VIZIWI) ambayo kitaifa maadhimisho haya yanafanyika Mkoani Shinyanga ndani ya halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
“ Ndugu zangu wananchi tunatarajia kuwa na uchaguzi wa serikali ya mitaa Novemba 27,2024 niwaombe sana kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura sambamba na kugombea nafasi husika kwa wenye sifa ili tuweze kupata viongozi wenye kuchochea maendeleo ya taifa letu”. amesema Mhe Macha.
Katika hatua nyingine Mhe. Macha,ameziagiza halmashauri zote mkoani humu, kila mwaka wa fedha kutenge bajeti ili kuwapeleka kozi maafisa uhusiano na Habari wa serikali, kusoma kozi za lugha ya alama,hali ambayo itasaidia watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) kupata mawasiliano na huduma stahiki.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Viziwi (CHAVITA) Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Frolah Nzelani amewataka wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa kusikia, kutowaficha badala yake wawaachie na kuwawezesha kushiriki katika mchakato wa uchaguzi.
Kilele cha maadhimishio haya kitaifa yatafanyika viwaja vya sabasaba Manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga Septemba 28,2024 yenye kauli mbiu “UNGANA KUTETEA HAKI ZA LUGHA YA ALAMA”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga