- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeendelea kung’ara katika sekta ya elimu baada ya hivi karibuni kushika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba (PSLE) mwaka 2025, kwa kupata ufaulu wa wa jumla wa asilimia 87.
Kutokana na mafanikio hayo, Idara ya Elimu ya Awali na Msingi ya Manispaa ya Shinyanga imeandaa hafla maalum ya kutunuku vyeti vya pongezi kwa walimu pamoja na shule za msingi zilizofanya vizuri katika PSLE na Mtihani wa Upimaji wa Darasa la Nne (SFNA) kwa mwaka 2025.
Akitoa taarifa ya matokeo hayo, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Awali na Msingi Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Mary Samson Maka, amesema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja kati ya walimu, wanafunzi, wazazi na wasimamizi wa elimu.
Ameongeza kuwa katika Mtihani wa Upimaji Darasa la Nne (SFNA), Manispaa ya Shinyanga imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa kupata asilimia 82.25 ya ufaulu wa jumla, hali inayoonesha mwelekeo mzuri wa elimu ya msingi kuanzia ngazi za awali.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndugu Revocatus Lutunda, amesema walimu ni nguzo muhimu katika maendeleo ya elimu na taifa kwa ujumla. Ametumia fursa hiyo kuwapongeza walimu kwa bidii na moyo wa kujituma, akisisitiza kuwa mafanikio hayo yanathibitisha kuwa uwekezaji katika elimu una tija kubwa.
Akikabidhi tuzo hizo Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Wakili Julius Mtatiro, amewapongeza walimu pamoja na Idara ya Elimu ya Awali na Msingi kwa ubunifu wa kuwapatia motisha walimu wanaofanya vizuri huku akiwashauri walimu kujifunza kutoka kwa shule zilizofanya vizuri zaidi ili kubadilishana uzoefu, kuongeza maarifa, mbinu bora za ufundishaji na kuimarisha ubunifu katika kuinua zaidi viwango vya elimu Manispaa ya Shinyanga.
Mafanikio haya yameifanya Manispaa ya Shinyanga kuendelea kuwa mfano wa kuigwa katika sekta ya elimu, yakionesha dhamira ya dhati ya Serikali katika kuboresha elimu kwa maendeleo endelevu ya jamii na taifa kwa ujumla.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga