- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MACHA AMPONGEZA MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA KWA USIMAMIZI MZURI WA USAFI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Na. Shinyanga MC
Manispaa ya Shinyanga yapongezwa kwa usimamizi mzuri wa Usafi wa miundombinu ya barabara pamoja na kusimamia usafi wa Manispaa hali iliyopelekea kuwa washindi wa tuzo ya usafi kwa mwaka 2024 ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo kushinda tuzo hiyo( 2023 na 2024)kati ya Manispaa 19 nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze , katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika leo tarehe 15 Julai, 2024 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wabunge, wakala wa barabara Nchini Mkoa wa Shinyanga (TANROADS) Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Shinyanga (TAKUKURU) pamoja na Wakala wa barabara Mijini na vijijini Mkoa wa Shinyanga (TARURA).
“Hongera sana Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kwa usimamizi mzuri wa usafi wa miundombinu ya barabara, Mitaro pamoja na mazingira kwa ujumla na ninyi Halmashauri zingine njooni mjifunze kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga”. amesema Mhe. Macha
Aidha Mhe.Macha ameagiza mabango yote yanayohusu ujenzi wa miradi ya barabara kwa lugha ya Kiswahili ili kuendelea kukuza na kuenzi lugha ya Taifa.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Macha amekemea tabia ya wananchi kujimilikisha maeneo ya hifadhi za barabara hususani wanaofanya biashara kandokando mwa barabara kinyume na utaratibu uliopangwa ikiwa kuna masoko husika kwa ajili ya kufanya biashara na sio kufanya kandokando ya barabara.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga