- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Maninspaa ya Shinyanga imekabidhi Pikipiki moja kwa Mtendaji wa Kata ya Mwawaza ambayo imetolewa na Serikali Kuu ikiwa ni sehemu ya Pikipiki zilizotolewa kwa ajili ya Watendaji Kata Nchi nzima kwa lengo la kuwarahisishia utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza wakati wa halfa fupi ya kukabidhi pikipiki hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amesema kuwa, anamshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwakumbuka Watendaji wa Kata ambao kwa sehemu kubwa wamekuwa wakishughulika na wananchi moja kwa moja.
Pamoja na maelekezo mengine, Mhe. Masumbuko amemtaka Mtendaji Kata huyo kwenda kuitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na kuhakikisha kuwa chombo hicho kinatunzwa zaidi na siyo kwenda kuitumia tofauti na maelekezo kusudiwa.
"Kwanza tunamshukuru sana Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwajali Watendaji wa Kata na hata kuwapatia vitendea kazi ambapo kwetu sisi Manispaa ya Shinyanga tumepata pikipiki moja ambayo leo hii tarehe 10/3/2023 tunamkabidhi Mtendaji Kata ya Mwawaza kwa kuzingatia Jiografia ya eneo hilo na kuwa sehemu kubwa ya makazi huko yametawanyika, hivyo chombo hiki kitaenda kusaidia kusogeza huduma karibu na wananchi na ndiyo kusudio la Serikali," amesema Mhe. Masumbuko.
Awali akimkaribisha Mhe. Masumbuko kukabidhi, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Manispaa ya Shinyanga Bi. Getrude Gisema alisema kuwa Manispaa imebahatika kupata mgawo wa pikipiki moja ambayo imekwishafika na ambayo atapatiwa Mtendaji Kata ya Mwawaza kwa kuzingatia eneo hilo lilivyo na mahitaji pia.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Mwawaza Ndg. Gaudios Mombeki alimshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa Watendaji Kata na hivyo kuamua kuwarahisishia kazi zao huku akiahidi kwenda kuitunza, kuongeza ufanisi wa kazi zake za kila siku kwa kuwafikia wananchi kwa urahisi na kwenda kuongeza ukusanyaji wa mapato sambamba na kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga