- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika zoezi la uandikishaji wa wanafunzi darasa la kwaza imeweza kuandikisha jumla ya wanafunzi 5,233 sawa na asilimia 99 huku makadilio ikiwa ni kuandikisha wanafunzi 5,288 kwa mwaka wa masomo 2025 wakitakiwa kuandikishwa.
Hayo yamebainishwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Ndg. Charles Luchagula ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni Sanaa na Michezo wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro kwenye kikao kazi maalumu cha uwasilishaji wa udahili na uandikishaji wa wanafunzi wa darasa la awali, darasa la kwanza na kidato cha Kwanza, kikao kilichofanyika Januari 30,2025 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga; Kikao kilichowakutanisha Wakuu wa Shule za Msingi na sekondari,Maafisa Elimu kata, Watendaji wa Kata, mitaa,na vijiji pamoja afisa utumishi kutoka manispaa ya shinyanga.
“Kwa mwaka wa masomo 2025 tumeandikisha Jumla ya wanafunzi wa darasa la kwanza 5,233 sawa 99% huku makadilio yakiwa ni kuandikisha wanafunzi 5,288 kwa mwaka huu, darasa la awali tumefanikiwa kuandikisha wanafunzi 4,2512 sawa na 72% idadi ikihitajika 5,936, huku Jumla ya wanafunzi 3,238 sawa na asilimia 73.4 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wameripoti huku makadilio yakiwa kuripoti wanafunzi 4,409”. Amesema Ndg. Luchagula
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro ameupongeza uongo wa manispaa kwa jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Manispaa Kuhakikisha Watoto hawazagai mtaani na kuwafanya wapate haki yao ya elimu , huku akiwataka kuongeza juhudi zaidi ya kuwasaka ambao hawajaripoti shule ikiwa nia pamoja na kuwachukulia hatua kali kwa wazazi wa Watoto hao.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga