- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI ya Usalama Wilaya ya Shinyanga ikiongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi Machi 9, 2023 imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiwa ujenzi wa Shule ya Sekondari Wasichana ya Butengwa ambayo bado inaendelea na ujenzi, ukarabati wa Bweni la Shule Maalumu ya Buhangija, ujenzi wa soko la wafanyabiashara wa bidhaa ndogo ndogo la Ibinzamata na soko la mtumba lilipo Kata ya Ngokolo pamoja na ujenzi wa jengo la Utawala lililopo katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Mwenyekiti wa kamati ya Usalama, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh. Johari Samizi (kushoto), akifanya ukaguzi wa Darasa la Shule ya Sekondari Butengwa
Akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Samizi aliitaka Menejimenti ya Manispaa kuhakikisha kuwa inazingatia ubora wa viwango vinavyohitajika katika kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda wa mikataba inayosainiwa wakati wa kuanza kazi hizo huku akimtaka Mhandisi Kassim Thadei wa Manispaa kuwa makini zaidi katika kusimamia miradi hiyo ya Manispaa kwani inatokana na kodi za wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.
Aidha wajumbe wa kamati ya usalama walishauri uwepo ukaguzi wa karibu na wa mara kwa mara katika kusimamia kazi hizo ambazo kwa mtazamo wa kawaida tuu ni kuwa umegharimu fedha nyingi sana na kwa sehemu kubwa inatekelezwa kwa mapato ya ndani ukiachilia mbali jengo la Utawala ambalo linatekelezwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu.
Ukaguzi uliofanywa na Kamati ya Usalama katika miradi ya maendeleo, ni utaratibu wa kawaida kabisa katika kuhakikisha kuwa kuna uwajibikaji wa kweli katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuri za kila siku katika Manispaa ya Shinyanga, jambo ambalo linapelekea kuwepo kwa imani kwa wananchi juu ya Serikali yao katika kuwapelekea huduma karibu yao zaidi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga