- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na Shinyanga MC
Kamati ya Lishe katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeweka mikakati zaidi katika kuboresha
utekelezaji wa shughuki zake kwa Kata zote 17 za Manispaa ikiwa ni pamoja na kuongeza utoaji wa
elimu kwa umma, kusimamia zoezi la utoaji wa chakula mashuleni, kuanzisha vitalu vya mbogamboga
katika shule zote kwa ajili ya wanafunzi kula mchana pamoja na kutekeleza kwa vitendo Siku ya Afya na
Lishe ambayo itakuwa ikifanyika katika ngazi za Vijiji, Mitaa na Kata.
Akielezea mikakati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Manispaa ya Shinyanga Ndg. Jomaary Mrisho
Satura ambaye ndiye Mkurugenzi wa Manispaa aliwaeleza wajumbe kuwa ni muhimu sana kwa kila
mjumbe kwenda kuisimamia ajenda ya Lishe kwenye eneo lake kwa umakini, weledi na ubunifu zaidi,
usimamizi na ufuatiliaji wa ulimaji wa viazi lishe pamoja na mambo mengine ili lengo la kukabiliana na
tatizo la Lishe kwa Manispaa ya Shinyanga lifikiwe kwa asilimia 100.
"Twendeni tukasimamie mambo yote yanayohusu Lishe ikiwa ni pamoja na kuanzisha, kusimamia na
kuboresha vitalu vya mbogamboga katika kila shule, utoaji wa elimu ya Lishe uwe endelevu, utoaji wa
chakula kwa kila shule, upimaji wanafunzi ili kujuwa afya zao, kuhuisha taarifa zote na ifike wakati sasa
Manispaa ya Shinyanga iwe kama Duka ambalo lina kila kitu ambacho wengine wanapokuja kujifunza
kwetu kila kitu wakikute kipo vizuri na kwa usahihi," alisema Satura.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Lishe kwa Manispaa ya Shinyanga kwa kipindi cha
robo ya pili 2022/2023 Afisa Afya na Lishe wa Manispaa Ndg. Amani Benson Mwakipesile alisema kuwa
Manispaa imetekeleza suala la kuhamasisha uzalishaji na unywaji wa maziwa ili kuboresha afya kwa
wananchi, kuhamasisha kilimo cha viazi lishe kayika Kata 1o kati 17 za Mansispaa.
Amani alisema kuwa, ukaguzi ulifanyika na unaendelea kufanyika katika Viwanda vyote kuhakikisha
kuwa kwenye kila uzalishaji wao wa vyakula kuna virutubisho vyote pamoja na madini joto, kuhakiki
Klabu za Afya Lishe na Mazingira katika Shule za Msingi zote, kubainisha watoto wote wenye utapiamlo
na kupatiwa matibabu, na umuhimumwa matone ya Viatmin A kwa chini ya watoto wenye umri chini ya
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga