- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC SAMIZI ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA SHINYANGA .
Na.Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi leo tarehe 10 Novemba, 2023 amefanya ziara ya kukagua na kutembelea Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akiwa katika ziara hii Mhe. Samizi ametembelea ujenzi wa nyumba za walimu katika shule ya sekondari Lubaga, ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana Shinyanga, ujenzi wa jengo la Utawala la Manispaa ya Shinyanga, pamoja na ujenzi wa shule ya sekondari Ngokolo B huku akiwataka wasimamizi wa miradi hii kusimamia miradi kwa usahihi kwani kila fedha zinazotoka Serikalini zinalenga kukamilisha kabisa mradi husika au kufikia hatua ya ukamilishaji, ambapo pia amewataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili majengo yakamilike kwa wakati.
"Niwatake muendelee kuzingatia matumizi mazuri ya fedha zinazoletwa kwa ajili ya miradi,Serikali inapoleta fedha hizi zinalenga kabisa kukamilisha mradi husika au kufikia katika hatua ya ukamilishaji lakini pia mafundi ongezeni kasi ya ujenzi ili majengo yakamilike kwa wakati" amesema Mhe. Samizi
Mhe. Samizi pia amesisitiza katika hatua ya ukamilishaji iwe ya ubora , kuweka samani za uimara kulingana na fedha zilizotolewa pamoja na kuweka samani zenye mfanano mmoja na sio ziwe tofauti.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Samizi amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa kuanza hatua ya kusajili shule mpya ya sekondari ya Ngokolo B inayoendelea kujengwa ambapo kwa mwakani inategemewa kupoke wanafunzi wa kidato cha kwanza 2024.
Ziara hii ya Mhe Samizi ni zaira ya kawaida yenye lengo la kukagua na kutembelea miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga