- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Ziara ya siku mbili kwa Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Tabora imekamilika leo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kutembea na kujifunza katika shughuli za uendeshaji wa miradi midogo na ya kati iliyopo katika eneo la Viwandani, uanzishwaji na utunzaji wa dampo lililopo Kizumbi uanzishwaji na uendeshwaji wa machinjio ya kisasa Ndembezi.
Akitoa salamu na ujumbe kutoka Manispaa ya Tabora, kaimu Mkurugenzi ndg Gudu Malulu aliwaeleza wenyeji kuwa lengo la kusafiri kwenda Shinyanga ni kujifunza namna ambavyo wamefanikiwa mambo mbalimbali kama yalivyotajwa hapo juu.
” Kwa dhati kabisa tumedhamiria kuja kujifunza na kuchukua yale yote yenye tija kubwa yatokanayo na ziara hii ili yaende kuwa msaada mkubwa kwa Manispaa yetu ya Tabora kwa muktadha wa kuipaisha Kiuchumi, kuboresha huduma za jamii, kuongeza na kuimarisha mapato na kimaendeleo kwa ujumla ili kufikia malengo ambayo Manispaa imejiwekea hasa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023”, alisema Malulu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg Jomaary Mrisho Satura alisema kuwa ni faraja sana kwa Wana Shinyanga kwa kutembelewa na ugeni kama huo muhimu jambo bora zaidi wenye lengo la kuja kujifunza mambo ambayo wameyaona ni mema kwao na yanapatika katika Manispaa ya Shinyanga, na kwamba aliwaahidi ushirikiano wa kutosha zaidi ili waridhike na wapate walichokusudia na kiende kuwa na matokeo chanya kwa wananchi wao.
Satura alisema kwamba Shinyanga siyo bora zaidi kuliko Halmashauri zingine, lakini kitendo cha Manispaa ya Tabora kuichagua Shinyanga ni jambo jema na lenye kuleta faraja kubwa sana, na kwamba Manispaa ya Shinyanga itakwenda kujifunza pia mambo mazuri kutoka Manispaa ya Tabora.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe Elias Masumbuko, aliwashukuru sana Waheshimiwa Madiwani Kutoka Manispaa ya Tabora kwa kuiona Shinyanga na hata wakaamua kwenda kujifunza, hivyo akawaomba kuwa huru kuuliza, kuhoji, kukosoa na kuboresha pale ambapo wanaona panafaa kwa kusudi la kuleta tija na kuwahudumia wananchi wa Manispaa ya Shinyanga.
“Siyo kwamba tuu mmekuja kujifunza kutoka kwetu, hapana nasi pia kupitia ujio wenu tutajifunza mambo mengi yaliyo mazuri zaidi ambayo mmekuja nayio na huenda sisi hatukuwa nayo pia, ndiyo maana nasema mkosoe, mshauri na mhoji kwa kadiri mtavyoona ili nasi tujikosoe pia,” alisema Meya Masumbuko.
Akifunga ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora, Mhe. Ramadhani Kapela aliwashukuru sana wana Shinyanga kwa ukarimu wao waliowapatia tangu kufika kwao hapo, ushirikiano waliowapatia kwenye ziara hiyo ya kujifunza mambo mbalimbali na kwamba akiwaahidi wajumbe wote kuwa watakwenda kuyafanyia kazi yote yale waliyojifunza ili yakalete mabadiliko chanya zaidi kwa wananchi wa Manispaa ya Tabora.
Kukamilika kwa ziara hiyo ya siku mbili katika Manispaa ya Shinyanga, kunatoa fursa sasa kwa wao Waheshimiwa Madiwani kwenda kuyachakata na kuyabadilisha yale yote waliyojifunza na kuyaona kwenye ziara hiyo ili yakaonekane kwenye madiliko ya vitendo na maisha ya wananchi wao wanaowaongoza kwenye maeneo yao, sambamba na kukuza pato la Manispaa, kuboresha huduma kwa jamii, kuibua na kusimamia miradi yao wenyewe.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora Ndg Gudu Malulu (wa kwanza kushoto) akitoa salamu na ujumbe kutoka Manispaa ya Tabora wakati wa utambulisho kwenye ukumbi wa Mikutano Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg Jomaary Satura (wa kwanza kushoto) akielezea jambo mbele ya wajumbe kabla ya kuanza ziara hawapo pichani.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Tabora Mhe. Ramadhani Kapela akiwashukuru Waheshimiwa Madiwani wa Shinyanga, Menejimenti na wote walioshiriki kukamisha ziara hiyo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga