- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wenyeviti na wajumbe wa Serikali za Mitaa waliochaguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024 leo Novemba 29, 2024 wameapishwa na Kamishna wa Viapo wakili Agness Mlimbi kiapo cha utii na uadilifu pamoja na Kiapo cha kutunza siri.
Viapo hivyo vimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano Shule ya Sekondari wasichana Shinyanga iliyopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza mara baada ya viapo hivyo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka viongozi hao waliochaguliwa katika nyadhifa mbalimbali kufanyakazi kwa kushirikiana ili kuleta maendeleo chanya katika maeneo yao.
“wananchi wamewaamini ndio maana wamewachagua kuwatumikia nendeni mkafanya kazi kwa kushirikiana, Imani yenu kwa wananchi ni kuwatumikia, kuwaletea maendeleo kwenye mitaa yao, pamoja na kutatua changamoto zinazo wakabiri.” amesema RC Macha.
Katika hatua nyingine RC Macha ametumia fursa hiyo kutoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi hao wa serikali za mitaa, ambapo amewataka kuhakikisha amani inakuwepo katika maeneo yao ya utawala,kusimamia miradi ya maendeleo,pamoja na kutambua mipaka yao ya kiutendaji kazi.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amesema uchaguzi umemalizia kwa amani ambapo jumla ya viongozi wa serikali za mitaa 570 wamechaguliwa kutoka vyama hivyo vya siasa , Chama cha Mapinduzi (CCM) kikishinda mitaa 55, Vijiji 17, Vitongoji 83 Huku Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikishinda kitongiji kimoja pekee cha Mwagala Kata ya Ibadakuli ndani ya manispaa hii, wanawake wakiwa ni asilimia 30% walio shinda uchaguzi huo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga