- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa Jengo la abiria na maboresho ya Uwanja wa ndege Katika kata ya Ibadakuli Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kufungua taa za kuongoza ndege ili uwanja huo uanze kutumika ikiwa upo Katika hatua za mwisho wa ukamilishaji.
Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema haya leo Feb 16,2025 alipotembelea Ujenzi wa jengo la abiri pamoja na ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege uliopo kata ya Ibadakuli Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, ambapo unatarajiwa kukamilika kwa 100% ifikapo mwezi wa nane 2025, mradi unaotekelezwa na kampuni ya China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) kutoka nchini china.
“Sina mashaka na kampuni ya CHICO imefanya kazi Katika maeneo mengi sana Katika Nchi yetu, anafanya kazi nzuri, bora, na yenye kuridhisha kulingana na mahitaji ya mradi, lakini nitoe maelekezo kwa mkandarasi fungeni taa mara moja Katika uwanja huu ili uanze kutumika, hatua iliyofikia inaruhusu kufanya kazi wakati mnapamalizia sehemu chache zilizo salia ,kukamilika kwa uwanja huu utasaidia kurahisisha usafiri wa mikoa mitatu kutoka Kanda hii ya Ziwa Victoria mkoa wa Shinyanga, Simiyu pamoja na Geita lakini pia kukuza Pato la mkoa huu”.
Amesema Mhe. Majaliwa.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Joel Mwambungu amesema uwepo wa mradi huo umesaidia kuajiri Jumla ya wananchi 160 ajira za mkataba.
Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu )Mhe. Patrobas P. Katambi amesema kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imejipanga Kuanzisha Ujenzi wa hospital Katika kati hii ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga itakayowahudumia wananchi pamoja na wahudumu wa uwanja wa ndege mara baada ya kukamilika kwa mradi wa uwanja huo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga