- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ndugu Albert G. Msovela ametoa wito wa kufanya kazi kwa bidii kwa watumishi wa Halmashauri ya Manispaa Shinyanga ili kumuwakilisha vizuri Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli katika kutoa huduma bora kwa wananchi. Alitoa wito huo katika ukumbi wa mikutano wa Lewis Kalinjuna uliopo ofisi za Manispaa katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017 ambayo ilianza tarehe 16 Juni 2017.
Aidha Katibu Tawala amewaambia watumishi wa Umma waendelee kufanya kazi kwa uwazi na kwa weredi ili wanapoelekea mwisho wa mwaka 2016/2017 waweze kufanya tathimini ya mipango iliyopangwa mwanzoni mwa mwaka. Ameeleza kuwa urasimu, matumizi mabaya ya madaraka, majungu kazini, mijadala na maneno yasiyo na tija yasiwepo katika utendaji kazi.
“Tusipoyatekeleza haya, hata majukumu yako haya hutaweza kuyatekeleza. Lazima mtumishi wa Umma utambue sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma inasemaje, tuko kwenye mamlaka ya Serikali za Mitaa, nini wajibu wetu?. Kuna matatizo mengi yametupata kutokana na kutokuzingatia kanuni, sheria na miongozo ya utumishi wa umma. Kwa hiyo niwaombe ndungu zangu watumishi tuzingatie sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika utumishi wa umma”. Alisema Katibu Tawala Mkoa.
Mkurugenzi wa Manispaa-Geoffrey Mwangulumbi akizungumza na watumishi wa Manispaa.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ndugu Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa watumishi wa Manispaa amezungumza na watumishi wa Manispaa kwa kusikiliza na kujibu maswali mbalimbali ya watumishi wa umma akishirikiana na wakuu wa Idara mbalimbali. Pia ametumia mkutano huo kuwaelimisha watumishi wa umma sera, sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma. Mkutano wa watumishi ulijumuisha makundi mbalimbali ya watumishi waliopo katika Halmashauri ya Manispaa wakiwemo Wakuu wa Idara na Vitengo, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule, Watumishi wote waliopo makao Makuu ya Halmashauri na Idara ya Afya, na Wakuu wa Vituo vya Afya.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma imekuwa na ujumbe wa “Ushirikishwaji wa Jamii-Vijana washirikishwe katika masuala ya kijamii barani Afrika” ambapo Manispaa ya Shinyanga iliongeza muda wa saa moja zaidi kila siku ili kutoa fursa zaidi ya kutoa huduma bora kwa wananchi. Sambamba na uongezaji wa muda wa kuhudumia wananchi, pia ofisi ya Manispaa ilijenga banda huru la kutoa elimu ya utumishi wa Umma katika viwanja vya Zimamoto, na kusikiliza maoni ya wananchi katika sehemu zinapotolewa huduma za maji katika kijiji cha Mwamagunguli na Mwamalili, kero za ardhi zilisikilizwa katika kijiji cha Nhelegani.
Watumishi wa Manispaa wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga