- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Watumishi wa Halmshauri ya Manispaa ya Shinyanga wapongezwa kwa kuandaa vizuri taarifa za kufunga hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha 2022/2023 .
Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 29 Agosti, 2023 na Ndg. Saidi Kitinga Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kupitisha taarifa za hesabu za mwisho zinazoishia Juni 30 katika mwaka wa fedha 2022/2023 katika ukumbi wa Lewis kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga .
Ndg. Kitinga ameleeza kwamba taarifa hiyo imeandaliwa vizuri na kuonesha kipimo cha utendaji kazi, na imeonesha wafanyakazi wanafanya kazi kwa ushirikiano, hali ambayo inaonekana kuna uhai katika Halmashauri.
"Document hii ya taarifa ya hesabu za mwisho jinsi mlivyoandaa ni kipimo cha utendaji kazi mzuri kwa watendaji wetu wa Halmashauri na wanafanya kazi kwa ushirikiano kwa hilo ninawapongeza " alisema Ndg. Kitinga
Pamoja na pongezi hizo Ndg. kitinga alisisitiza zaidi kukamilisha miradi viporo, kushughulikia Mali chakavu ili kutoongeza thamani ya uchakavu pamoja na kutoa hamasa ya ukusanyaji wa mapato kwa watumishi.
Awali Ndg. Wallace Kiondo Kaimu Mwekahazina wa Manispaa ya Shinyanga akiwasilisha taarifa hizo za hesabu za mwisho zinazoishia 30 Juni mwaka huu ,Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilibaki na jumla ya Tsh bilioni 3.470,181,175 ambazo ni fedha zilizokuwa hazijatumika katika ngazi ya Halmashauri na ngazi ya chini ya Halmashauri ambapo katika fedha hizo Tsh. Milioni 963.434,484 ni fedha za bakaa ngazi ya Halmashauri na Tsh bilioni 2.506,746,691 fedha za bakaa ngazi ya chini.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga