- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WATENDAJI WA KATA,MITAA NA KIJIJI MANISPAA YA SHINYANGA WAPEWA MAELEKEZO YA KUKUSANYA TAKWIMU ZA MABANGO NA NYUMBA ZISIZOKUWA NA UMEME.
Na. Shinyanga Mc
Watendaji wa kata , vijiji na Mtaa leo tarehe 14 March, 2024 wameketi kwenye kikao kazi chenye lengo la kupatiwa maelekezo ya kwenda kukusanya takwimu za nyumba zisizokuwa na umeme na mabango katika ukumbi wa lewis kalinjuna katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
Akiwasilisha maelekezo hayo afisa biashara Ndg. Victor Kajuna amewaeleza kwamba serikali imefanya marekebisho mbalimbali ya sheria ya fedha ambayo yamerejesha usimamizi wa vyanzo vya kodi ya majengo na ushuru wa mabongo kwenye mamlaka ya serikali za mitaa ambapo hapo awali vilikuwa vinasimamiwa moja kwa moja na serikali kuu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA).
Aidha, ameeleza kodi ya majengo imegawanyika katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni nyumba zote zenye umeme ambazo kwa sasa zinatozwa kodi ya majengo kupitia mfumo wa LUKU , kundi hili litaendelea kutozwa kodi ya jengo kupitia TANESCO, na kundi la pili ni nyumba zisizokuwa na umeme ambapo mamlaka ya serikali za mitaa zimeelekezwa kuzitambua na kisha kuzitoza kodi ya majengo kulingana na aina ya nyumba na kiwango kilichoainishwa.
Ndg. Kajuna aliendelea kueleza kwamba utambuzi wa nyumba zisizo na umeme unazingatia makundi matatu, kundi la kwanza nyumba za kawaida, kundi la pili nyumba za kwaida zaidi ya moja kwenye kiwanja kimoja na kundi la tatu ni nyumba za ghorofa, huku katika ushuru wa mabango takwimu zitakusanywa kwa kuzingatia aina ya bango.
Pamoja na mambo mengine watendaji walipata wasaa wa kupewa muongozo wa namna ya kusimamia na kuunda mabaraza ya usuluhishi ya kata na Bi Rose Matunda Mwanasheria Manispaa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga