- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WATENDAJI MANISPAA YA SHINYANGA WAANZA MAFUNZO YA MFUMO WA FFARS.
Na. Shinyanga Mc
Watendaji wa Kata, Mtaa na Vijiji wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 22 Septemba, 2023 wameanza Mafunzo ya Mfumo wa Malipo Ngazi ya Vituo vya kutolea huduma, ofisi za Kata, Mitaa na Vijiji (FFARS) katika ukumbi wa shule ya msingi Buhangija katika Kata ya Ibinzamata.
Akizungumza katika ufungunzi wa mafunzo hayo Ndg. Mulokozi Kishenyi ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Manispaa ya Shinyanga amewaeleza washiriki wa mafunzo haya kuwa Serikali imeleta mfumo huu ili kurahisisha kazi katika utendaji kazi, kuimarisha usimamizi mzuri wa fedha na kusaidia ufuatiliaji pamoja na utoaji wa taarifa za fedha za miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa maeneo mbalimbali nchini kwa urahisi.
"Kutokana na uwepo wa mfumo huu, usimamizi wa fedha za umma umeimarika, upatikanaji wa taarifa za fedha umeimarika, uunganishaji wa taarifa za fedha za Serikali (final Account) umeimarika, utekelezaji na ukamilishaji wa miradi ya Serikali umeimarishwa pamoja na udhibiti wa ubadhilifu wa fedha za miradi umeimarishwa" alisema Ndg. Kishenyi
Ndg. Kishenyi amewaeleza washiriki kuwa kutokana na umuhimu wa mfumo huo, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imeamua kuanza kuutumia mfumo wa FFARS kwenye ngazi za Kata, Mitaa na Vijiji ili matumizi ya fedha zote za Umma yafanyike kupitia mfumo na hivyo kuzidi kuimarisha usimamizi, ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za fedha za Umma kila ifikapo mwisho wa mwaka.
Sanjali na hilo, Ndg. Kishenyi amewasisitiza washiriki wa mafunzo haya kufuatilia kwa umakini mafunzo ili baada ya mafunzo waanze kuutumia mfumo katika kupokea fedha na kufanya malipo mbalimbali, kwani baada ya mafunzo hayo hakuna malipo yatakayofanyika nje ya mfumo.
Kupitia mfumo huu wa FFARS unaenda kurahisisha kazi kwa watendaji katika malipo mbalimbali na kusaidia Serikali kupata taarifa za fedha zenye usahihi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga