- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WATAALAM WA KUTOA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA WAPATIWA MAFUNZO MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Wataalam wa kutoa chanjo ya surua na rubella wapatiwa mafunzo leo tarehe 14 Februari, 2024 katika ukumbi wa Lewis kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
Akifungua mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt.Elisha Robert amewataka wataalam hao kwenda kutoa chanjo kwa watoto wote waliochini ya miaka 5 ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika Manispaa ya Shinyanga.
“ Niwaombe wataalam wote mkatoe chanjo kwa kuzingatia umri wa watoto uliopangwa pamoja na kutoa kwa weledi ili tufikie malengo kwani kwa Manispaa yetu tunahitajika kuwafika watoto 24047” amesema Dkt. Robert
Kwa upande wake Ndg. Ramadhani Maneno Mratibu wa huduma za chanjo Manispaa ya shinyanga amewasihi wataalam wote kwenda kutoa chanjo kwa kuzingatia taratibu zote walizopatiwa ili kuepuka usumbufu wowote utakao jitokeza.
Chanjo ya Surua na Rubella itaanza rasmi kesho tarehe 15 mpaka 18 Februari, 2024 katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya, mashuleni, maeneo yenye watu wengi pamoja na masokoni.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga