- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WANANCHI MANISPAA YA SHINYANGA WAASWA KUCHANGAMKIA MIKOPO YA ASILIMIA 7 ILI KUJIKWAMUA KIUCHUMI.
Na: Shinyanga MC
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imetoa Elimu ya mkopo wenye riba nafuu, mikopo ya riba ya 7% yenye lengo la kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wadogo, kujikwamua kiuchumi, kukuza mitaji yao na kuondokana na umaskini.
Akizungumza katika kikao cha wafanyabiashara kilichofanyika leo Mei 14, 2025 katika Soko la Ngokolo mtumbani, Mratibu na Msajili wa Wafanyabiashara Wadogo Mkoa wa Shinyanga, Bi. Rose Tungu, ameeleza kuwa mfanyabiashara yeyote mdogo anapaswa kuwa na kitambulisho cha ujasiriamali ili kunufaika na mkopo huu unaotolewa kuanzia kiasi cha shilingi 50,000 hadi shilingi milioni 4.
“Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameona si vyema wananchi kuendelea kutegemea mikopo ya ‘kausha damu’ ambayo huwasababishia usumbufu na msongo wa mawazo. Kwa kutambua hilo, amehakikisha mikopo ya asilimia 7 inapatikana kupitia Wizara yetu, ili kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo kuinuka kiuchumi bila changamoto kubwa ya marejesho,” amesema Bi. Rose.
Naye Bi. Vaileth Mambosasa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi na wajasiriamali wadogo kujitokeza kwa wingi kuchangamkia mikopo hiyo ambayo inalenga kuwakwamua kiuchumi na kuwaondoa kwenye wimbi la umasikini.
Katika hatua nyingine, Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Kitengo cha Makundi Maalum, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Ndg. David Malebeto, alisema kuwa kwa Manispaa ya Shinyanga pekee, kiasi cha shilingi milioni 140 kimetengwa kwa ajili ya kuwawezesha wafanyabiashara wadogo kupata mikopo hiyo.
Nao baadhi ya wajasiriamali wa Manispaa ya Shinyanga wameishukuru Serikali kwa kuendelea kuthamini jitihada zao na kutoa mikopo hiyo ambayo imesaidia kuongeza mitaji yao, kuboresha maisha yao na kupambana na umasikini.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga