- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WANAFUNZI WA KIJESHI KUTOKA CHUO CHA CSC ARUSHA WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO YA NDANI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Wanafunzi wa Chuo cha Kimataifa cha kijeshi kinachotoa mafunzo kwa Maafisa wakuu wa Jeshi kutoka Mataifa mbalimbali kwa ngazi ya cheo cha Meja na kuendelea katika Chuo cha Ukamanda na Unadhimu Duluti Mkoani Arusha leo tarehe 9 Oktoba, 2023 wamefanya ziara ya mafunzo ya ndani katika Manispaa ya shinyanga.
Akitoa salam za Chuo Kanali Khamis Ngoi Mkuu wa msafari alieleza kuwa wamekuja Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kiutawala pamoja na shughuli za maendeleo ya kijamii na uchumi yanavyoweza kuhuishwa ili kuleta amani na usalama.
"Tumekuja Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali lakini pia tumeichagua manispaa ya shinyanga kuwa sehemu yetu ya mafunzo kwasababu manispaa ya shinyanga imekaa kimkakati na inazo rasilimali za kutosha kwa ajili ya kujifunzia" alisema Kanali Ngoi
Wakiwa Manispaa ya Shinyanga Wanafunzi hao wa kijeshi waliweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mambo ya kiutawala, shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanavyoweza kuhuishwa ili kuendana sawa na masuala ya amani na usalama , namna ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mapato ya ndani pamoja na mila na desturi za watu wa mkoa wa shinyanga.
Sanjali na hilo , Wanafunzi hao wakijeshi waliweza kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo shule mpya ya msingi ibadakuli, soko la mitumba ngokolo, kituo cha afya kambarage na soko kuu la shinyanga.
Aidha kwa Upande wa Manispaa ya Shinyanga timu iliongozwa na Mhe. Zamda Mwebea Naibu Meya Manispaa ya Shinyanga pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo iliwashukuru kwa kuichagua Manispaa ya Shinyanga kama sehemu yao ya kujifunza na kwamba uongozi wa Manispaa pamoja na mambo mengine umewakaribisha wakati wowote.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga