- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WALIMU WA MALEZI SHULE ZA MSINGI,SEKONDARI NA VYUONI MANISPAA YA SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO YA KLABU ZA MAADILI.
Na. Shinyanga Mc
Walimu wa Malezi shule za Msingi, Sekondari na Vyuoni Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 23 Oktoba, 2023 wamepatiwa mafunzo ya uanzishwaji wa klabu za maadili katika ukumbi wa Ofisi za Tarula Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumzo katika ufunguzi wa mafunzo haya Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Ndg. Ibrahim Makana amesema lengo la Klabu za Maadili ni kuwajengea wanafunzi na wanavyuo misingi bora ya maadili kuanzia mashuleni mpaka wanapofika vyuoni.
“Lengo la klabu za maadili mashuleni na vyuoni ni kuwajengea wanafunzi kuwa na nidhamu nzuri kuanzia wanapokuwa shule mpaka wanapofika vyuoni ili kujenga kizazi chenye maadili mema “amesema Ndg. Makana
Kwa Upande wake Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Gerald Mwaitebele amesema Klabu hizi zitasaidia kuwajengea wanafunzi kujua maadili yanayopaswa kuzingatiwa katika ujenzi wa Taifa letu pamoja na kuwa mzalendo wa kweli katika Taifa ili kuweza kupata viongozi wenye maadili na kizazi chenye uadilifu, huku akiwata walimu kutumia vikao vya wazazi mashuleni kufikisha ujumbe wa mambo ya maadili kupitia klabu walizozianzisha.
Aidha, Ndg. Mwaitebele ameeleza sifa za mwalimu anayefaa kuwa mlezi katika klabu za maadili ikiwemo Mwadilifu, Mwaminifu, Muwazi,Mzalendo, Mchapakazi na anayekubalika kimaadili na wanafunzi.
Pamoja na mambo mengine Timu ya Waratibu wa Mafunzo haya ikiongozwa na Ndg. Mwaitebele ilipata wasaa wa kutembelea shule mbalimbali ambazo tayari zimeanzisha klabu za maadili ikiwemo Shule ya sekondari Chamaguha, shule ya sekondari Uhuru, shule ya msingi Jomu, shule ya msingi Town, shule ya msingi Kambarage pamoja na shule ya msingi uhuru ambapo wanafunzi waliandaa nyimbo na maigizo mbalimbali yenye kuhamasisha maadili mema.
Kuanzishwa kwa Klabu za maadili mashuleni na vyuoni kunaenda kuwasaidia wanafunzi kutoka katika tabia hatarishi na kuwasaidia wanafunzi kupata maadili mema kuanzia nyumbani mpaka vyuoni na kuleta picha nzuri katika jamii wanazoishi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga