- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kuimarisha uwajibikaji na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma, Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu matumizi ya Mfumo wa kujibu hoja kwa njia ya Kielektroniki (IFTMIS) wa ukaguzi na ufuatiliaji fedha kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa.
Akifungua rasmi mafunzo haya, leo tarehe 25 Aprili 2025, katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Peres Kamugisha amesisitiza umuhimu wa viongozi hao kuwa na uelewa wa kina wa mfumo huo ili kuongeza uwazi na ufanisi katika kushughulikia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
“Mfumo huu ni chombo muhimu katika kuhakikisha tunatekeleza hoja za CAG kwa wakati na kwa ufanisi.lengo kuu ni kuelewa matumizi sahihi ya mfumo, ili iturahisishie katika ufanya kazi kwa wakati na kwa haraka kwa maslahi mapana ya Halmashauri yetu” amesema ndg. Kamugisha.
Mafunzo haya yanatarajiwa kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa Halmashauri, sambamba na kuhakikisha hoja zote za CAG zinatekelezwa kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga