- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko ameagiza wafanyabisha wote ambao wanafanya biashara sehemu ambazo sio rasmi warudi na wafanye katika maeneo yalitengwa kwa ajili ya biashara .
Agizo hili amelitoa leo tarehe 31 Oktoba, 2023 katika Baraza la Madiwani robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 baada ya kuwasilishwa taarifa ya kamati ya fedha na utawala na kuagiza wafanyabishara wote wanaofanya biashara sehemu zisizo rasmi warudi kufanya biashara katika sehemu zilizotengwa ili kuweza kukusanya mapato kwa urahisi.
"Wafanyabiashara wote warudi katika sehemu rasmi zilizotengwa kwa ajili ya kufanyia biashara" amesema Mhe. Masumbuko
Awali Mhe. Masumbuko aliainisha maeneo ambayo ni rasmi kwa ajili ya biashara ni soko la mbao la Chamaguha maalum kwa ajili ya kuuzia mbao na Milunda pamoja na Soko la Mitumba Ngokolo kwa ajili ya kuuzia nguo za Mitumba.
Aidha, agizo hili baada ya kutolewa na Mhe. Masumbuko Baraza la Madiwa kwa ujumla limekubali na kuazimia agizo hili ili kuweka urahisi na kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Masumbuko alimpatia zawadi ya tishrt Mkuu wa msafara wa wageni walitoka Nchi ya Mozambique ambao walipata wasaa wa kujitambulisha katika baraza la madiwani.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga