- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wadau wa Mradi wa Elimu Jumuishi wamekutana Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa lengo la kuendesha warsha ya uboreshaji mkakati wa ushirikishwaji wa mashirika ya watu wenye ulemavu katika program ya Elimu jumuishi kwa lengo la kujadili namna ya kutokomeza ukatili kwa watu wenye ulemavu.
Warsha hii imefanyika leo septemba 9, 2024 katika hoteli ya karena Manispaa ya Shinyanga iliyowakutanisha Maafisa Elimu Maalum, Maafisa Habari, Maafisa Ustawi wa Jamii Pamoja na watu wenye ulemavu kutoka Halmashauri tatu, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Misungwi kutoka Mkoa wa Mwanza ambapo Mradi huu unatekelezwa katika maeneo hayo.
Akizungumza katika Warsha hii mwezeshaji Bi. Anasteria Gwajima ambaye ni mratibu wa maswala ya jinsia amesema kuwa kuna baadhi ya wanaume wanakimbia familia zao kwa kigezo cha kupata mtoto mwenye ulemavu huku akilaani wale wanaotumia majina kandamizi kwa watu wenye ulemavu.
“Sisi sote ni walemavu watarajiwa, kuzaliwa mlemavu sio dhambi maana ni kazi ya Mungu, kuna baadhi ya wanaume wanakimbia familia zao pale mama anapojifungua mtoto mwenye ulemavu wakidai kuwa mtoto mwenye ulemavu ni laana vitendo vya namna hiyo havifai kwenye jamii zetu”. amesema Bi.Gwajima
Mradi wa Elimu Jumuishi unatekelezwa na umoja wa mashirika manne, ADD International, Light for the World, Sense International na Tanzania Cheshire Foundation ukikutanisha mashirika ya watu wenye ulemavu pamoja na baadhi ya Maafisa wa Serikali.
Warsha hii inafanyika kwa siku mbili katika Manispaa ya Shinyanga kuanzia leo tarehe 12 septemba mpaka 13 Septemba 2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga