- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Afisa Mwandikishaji msaidizi jimbo la Uchaguzi Shinyanga Mjini Bw.Charles Kafutila amewataka waandishi wasaidizi na maendeshaji vifaa vya Bayometriki kushirikiana kikamilifu na maafisa waandikishaji wasaidizi kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi Mzuri kuelekea kwenye uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Kafutila ameyasema haya leo Agosti 18,2024 wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wasaidizi na waendeshaji vifaa vya Bayometriki jimbo la shinyanga Mjini, mafunzo yatakayofanika kwa siku mbili katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Uwalimu Shinyanga SHYCOM.
“Niwasihi muwe na Ushirikiano wa karibu na Maafisa waandikishaji ngazi ya kata, pale mnapopata changamoto yoyote wasiliana na maafisa waandikishaji waliopo kwenye kata zetu ili tuweze kufanya kazi hii kwa ufanisi zaidi amesema” Bw. Kafutila
Zoezi hili limeenda sambamba na viapo viwili kiapo cha kutotoa siri Pamoja na kiapo cha kujitoa katika chama chochote cha siasa wakati wa mkataba kwa waandishi wasaidizi na waendesha vifaa vya Bayometriki.
Mafunzo haya yamejumuisha wataalamu kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Maafisa uchaguzi ngazi ya Mkoa, Pamoja na Halmashauri ambao walikuwa wakitoa mafunzo kwa waandishi wasaidizi na waendeshaji vifaa vya Bayometriki ambao watakwenda kusimamia na kuendesha zoezi la uandikishaji na uboreshajui wa daftari la kudumu la wapiga kura ambapo kwa jimbo la Shinyanga Mjini zoezi hilo litaanza kutekelezwa tarehe 21 hadi 27, Agosti 2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga