- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
"WAAJIRI SIMAMIENI STAHIKI ZA MAKATIBU MAHSUSI" RC MNDEME
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaagiza waajiri wa Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha wanasimamia stahiki zote za makatibu mahsusi .
Agizo hilo amelitoa leo tarehe 7 Novemba, 2023 wakati akifungua kikao kazi cha kuzindua chama cha makatibu mahsusi (TPSEA) mara baada ya kupokea risala ya wanachama hao ambapo ndani yake ilielezea changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa stahiki zao kama kuhudhuria mafunzo na mikutano mbalimbali inayohusu taaluma yao.
"Nimesikiliza kwa makini risala yenu nichukue nafasi hii kuwaagiza waajiri wote kusimamia stahiki za makatibu mahsusi ikiwemo kutenga bajeti ya kuhudhuria mafunzo na mikutano mbalimbali inayohusua taaluma yao pamoja na kuwapatia ruhusa ya kushiriki mafunzo na mikutano hiyo." amesema Mhe. Mndeme
Aidha, Mhe. Mndeme ameendelea kusisitiza kuwa makatibu mahsusi ni watu muhumu sana katika ofisi wanabeba siri nyingi pamoja na kujua mambo mengi yanayohusu ofisi, mtu akiwadharau makatibu mahsusi basi atakuwa hajitambui.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mndeme amewasihi makatibu mahsusi kupata muda wa kujiendeleza vizuri kielimu ili wawezi kuwa viongozi mbalimbali Kitaifa
Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA) kina jumla ya wanachama
118 kutoka Taasisi za Serikali na umma Mkoani Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga