- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius S. Mtatiro ametoa maagizo kwa watendaji wa Kata, vijiji, mitaa na vitongoji, maafisa Elimu Msingi na sekondari kata, Waratibu Elimu Msingi na sekondari ngazi ya kata Kuhakikisha watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato Cha kwanza 2025 pamoja na watoto waliofika umri wa kuanza Darasa la awali na Msingi wanaandikishwa ndani ya muda.
Wakili Mtatiro ametoa maagizo hayo Leo Januari 10,2025 kwenye kikao kazi na Walimu wakuu Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na binafsi, Waratibu Elimu, Maafisa Elimu Msingi na Sekondari, watendaji wa Kata, vijiji, mitaa na vitongoji kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kikao kilichofanyika Ukumbi wa mikutano Shule ya wasichana Shinyanga iliyopo kata ya Butengwa kata ya Ndembezi.
“Isitokee kesi yoyote kwa mzazi kuzuiwa mtoto wake kujiunga na kidato Cha kwanza eti kwa kigezo Cha hana sare za shule, wanafunzi wote wapokelewe, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Mpendwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya kila liwezekanalo ili kuweka mazingira na miundombinu bora zaidi ya kuwapokea wanafunzi wa Darasa la awali na Msingi kwenye kila shule kulingana na hali na mazingira waliyonayo, ninyi mkiwa viongozi mlio karibu sana na jamii niwaombe nendeni mkatoe ushirikiano wa hali ya juu ili tuhakikishe Watoto wote wanapata Elimu”.Amesema Wakili Mtatiro.
Katika hatua nyingine Wakili Mtatiro amewataka walimu wakuu Kuhakikisha katika muhula huu wa masomo wanasimamia na kutoa mitihani ya mara kwa mara ya ndani ili kuwawezesha wanafunzi kuwa na kiwango kizuri Katika mitihani yao ya kitaifa.
Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kwa mwaka wa masomo 2025 imejipanga kuandikisha Jumla ya wanafunzi wa Darasa la awali 5,936, huku darasa la kwanza na Msingi 5,288 huku kidato cha kwanza Jumla ya wanafunzi 4,274 wavulana wakiwa ni 1,867 na Wasichana wakiwa 2,407.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga