- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
VIONGOZI MANISPAA YA SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA PAMOJA NA MAADILI KWA VIONGOZI WA UMMA.
Na. Shinyanga Mc
Viongozi Halmshauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwemo Waheshimiwa Madiwa, Watendaji wa Kata, Mitaa na vijiji leo tarehe 8 Novemba, 2023 wamepatiwa mafunzo ya kuzuia na kupambana na rushwa pamoja na maadili kwa viongozi wa umma katika ukumbi wa kalinjuna uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akifungua mafunzo haya kaimu Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu Ndg. Stephen Okoth amewataka washariki kusikiliza kwa makini huku akiwaeleza kuwa wajibu wa kuzuia na kupambana na rushwa si (TAKUKURU ) bali ni jukumu la jamii nzima pamoja na maadili kwa viongozi wa umma ni wajibu wa kila mtumishi wa umma.
"Niwaombe washiriki muwe wasikivu katika mafunzo haya na tutambue kuwa swala la kupambana na kuzuia rushwa sio TAKUKURU tu bali ni jukumu la jamii nzima pia maadili kwa kila kiongozi ni jukumu la kila mmoja wetu."amesema Ndg. Okoth
Kwa Upande wake Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Ndg. Gerald Mwaitebele ameeleza kwamba ikiwa wanaelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Maadili kitaifa ambapo kilele chake ni tarehe 10 Novemba, 2023 basi wameamua kuja kutoa mafunzo kwa viongozi ili waweze kuwakumbushia sheria ya maadili ya viongozi wa umma, maadili katika sekta ya umma pamoja na mgongano wa maslahi katika utumishi.
Aidha, akiongea katika utangulizi wa mafunzo haya naye Ndg. Mohamed Doo Afisa Uchunguzi TAKUKURU Mkoa wa shinyanga, amewaeleza washiriki kuwa lengo la mafunzo haya ni kubadilishana uzoefu ili kuwawezesha viongozi kuwa na uelewa utakao wasaidia kujua rushwa, madhara yake katika kazi hasa wanapohudumia jamii na njia ya kuiepuka.
Kila kiongozi wa umma au mtumishi anapaswa kuhakikisha kuwa anatoa huduma ipasavyo bila kutegemea kupewa zawadi kama asante kwani inamfanya mtoaji au mpokeaji kujenga tabia ya kutegemea zawadi ili atoe au apokee huduma jambo ambalo hupelekea rushwa swala ambalo ni kosa na si maadili kwa mtumishi wa umma.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga