- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
UONGOZI WA TIMU YA JKT WAFIKA OFISI YA MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA KUJITAMBULISHA
Na. Shinyanga Mc
Uongozi wa Timu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo tarehe 28 Septemba, 2023 wamefika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa lengo la kujitambulisha.
Ambapo Mwenyekiti wa Timu hiyo ya JKT Capt. Godwin Ekingo aliongozana na Mwenyekiti wa chama cha mpira Shinyanga Ndg. Said Mankilingo, Afisa Michezo Mkoa wa Shinyanga Bi Jesca Simuchile pamoja na Masau Bwire kiongozi wa timu ya JKT.
Lengo la uongozi huo kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni kujitambulisha na kuitambulisha timu ya JKT ambayo kwa sasa imepanda daraja na kwa mwaka huu itacheza ligi kuu Nchini na kesho tarehe 29 Septemba, 2023 itachuana na kagera Sugar katika viwanja vya CCM Kambarage Shinyanga.
Aidha, Viongozi hao waliiomba Serikali kuendeleza mahusiano mazuri katika kutoa ushirikiano kwenye timu za mpira pamoja na katika kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mechi mbalimbali.
Kwa Upande wake Mhe. Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga amewapokea kwa mikono miwili na kuwaahidi kuwapa ushirikiano muda wowote na wakati wowote.
Timu ya JKT imechagua kiwanja cha CCM Kambarage kuwa ni uwanja wa nyumbani ambapo kesho watacheza na Kagera Sugar na tiketi za mechi ya kesho zinapatika VVIP na VIP ni Tsh 3000/= na sehemu ya kawaida bei Tsh 2000/=
Aidha, tiketi hizo zinapatika chini ya uratibu wa TTCL Shinyanga katika maeneo ya Uwanja wa Kambarage getini, eneo la Soko Kuu pamoja na Standi ya Wilaya .
Pamoja na Mambo mengine uongozi wa Timu ya JKT wameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa wilaya pamoja na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa kwa kufanya marekebisho ya kiwanja cha Kambarage na hatimaye ukakubaliwa na kuruhusiwa kutumika kwa mashindano ya ligi kuu Tanzania Bara.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga