- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake dunuani ambayo huadhimishwa kila ifikapo machi 08 ya kila mwaka, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kutambua umuhimu wa afya ya mama na mtoto ilifanya maadhimisho kwa ngazi ya Halmashauri machi 03,2025 maadhimisho yaliyoambatana na uchangiaji damu, usafishaji mazingira na kutoa misaada katika wodi ya wazazi kituo cha afya Kambarage ndani ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza leo machi 04, 2025 Muunguzi mfawidhi wa kituo cha afya Kambarage Bi. Paulina Kitambi amesema katika maadhimishi hayo jumla ya wananchi 40, walijitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya mama na mtoto ambapo jumla ya uniti 40 za damu zilichangiwa.
Katika hatua nyingine Bi. Paulina amewashukuru wanawake wa Manispaa ya Shinyanga kwa namna walivyojitoa ili kuokoa maisha ya mama na mtoto huku akitumia fursa hiyo kuwasihi wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kuendelea kujitokeza kuchangia damu ili kuokoa maisha ya kinamama pindi wanapojifungua.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa ngazi ya Mkoa yanatarajiwa kuadhimishwa machi 06, 2025 katika Halmashauri ya wilaya ya Msalala ambapo yataambatana na kaulimbiu isemayo. “wanawake na wasichana 2025: tuimarishe haki, usawa na uwezeshaji”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga