- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo kwa Maofisa Utumishi wa Sektretarieti ya Mkoa wa Shinyanga na Mamlaka zake sita za Serikali za Mitaa kuhusu uhakiki wa watumishi kwa kutumia taarifa za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) yamefanyika tarehe 13 Juni 2017 katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga. Jumla ya Maofisa Utumishi 13 kutoka katika Mkoa na Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga wamepata mafunzo ya kuhakiki watumishi kwa kutumia fomu na ripoti za NIDA zilizojengwa kwenye mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS). Halmashauri zilizoteua Maofisa utumishi kuhudhuria mafunzo ya uhakiki kwa muda siku moja ni Halmashauri ya Wilaya Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga, Kishapu, Msalala, Ushetu na Kahama Mji.
Ndugu Lenard Tumua-Ofisa kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma akitoa mafunzo kwa Maofisa Utumishi
Baada ya Mafunzo hayo ambayo yamehusisha Ofisa kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ndugu Lenard Tumua, zoezi la uhakiki wa watumishi limeanza mara moja kuanzia tarehe 14 Juni 2017 kwenye Halmashauri zote za mkoa wa Shinyanga ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na linasimamiwa na kutekelezwa na Maofisa Utumishi waliopata mafunzo. Aidha kila mtumishi anatakiwa kuwa na kitambulisho cha kazi chenye picha ya mtumishi, hati ya malipo ya mshahara na kitambulisho cha taifa ili aweze kuhakikiwa.
"Watumishi wote wa serikali ambao vituo vyao vya kazi vipo nje ya makao makuu ya taasisi zao kama vile polisi na magereza, watahakikiwa katika wilaya wanazofanyia kazi chini ya usimamizi wa Wakurugenzi wa Halmashauri ambako zoezi la uhakiki unafanyika". Alisema Ndugu Lenard Tumua wakati wa mafunzo kwa maofisa Utumishi.
Taasisi zinazohusika na zoezi la uhakiki wa watumishi ni zile ambazo watumishi wake wanalipwa mishahara kupitia mfumo wa taarifa za Kiutumishi na Mishahara.
Maofisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga baada ya mafunzo
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga