- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini Mwl.Alexius Kagunze amewataka viongozi na wadau wa vyama vya siasa huwahimiza wananchi na wachama, Pamoja na wafuasi wao wenyesifa kujitokeza kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwa ni pamoja na uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura serikali za mita ambalo linatarajiwa kuanza kufanyika Oktoba 11 hadi 20, 2024.
Mwl. Kagunze ameyasema haya leo Septemba 26,2024 wakati akizungumza na wadau na viongozi wa vyama vya siasa Jimbo la Shinyanga Mjini juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
“Ndugu zangu viongozi wa vyama vya siasa kwa mujibu na taratibu za tume huru ya taifa ya uchaguzi kuanzia tarehe 11 hadi 20 mwezi wa kumi tutakuwa na uandikishaji wa daftari la wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa, hivyo niwaombe sana muende kuwahamasisha wananchi kwa wenye sifa wote wajitokeze kujiandikisha sambamba na kuchukua fomu za kugombea ili tuweze kupata viongozi bora na si bora kiongozi, kwa maslahi mapana ya taifa letu”.amesema Mwl. Kagunze.
Aidha Mwl. Kagunze ameongeza kuwa uchaguzi wa serika za mitaa kwa mujibu wa tume huru ya taifa ya uchaguzi kanuni ya 15 GN Na 573 wanachi wenye umri wa miaka 21 na zaidi wajitokeze kuchukua fomu za uenyeviti wa vijiji ujumbe wa halmashauri ya Kijiji, uenyekiti wa kitongoji, mitaa,na ujumbe wa kamati ya mtaa.
Kwa upande wake Mkaguzi wa Uhamiaji mkoa wa shinyanga Bi. Elizabeth Kaka amesema kila mwananchi anayetaka kugombea au kujiandikisha kuwa mpiga kura kwa mujibu wa sheria ya nchi ya mwaka 1995 No. 6 lazima awe raia wa Tanzania ,uraia wa Kuzaliwa, Kurithi Pamoja na Uraia wa kujiandikisha.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga