- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
TUMIENI LUGHA NZURI MNAPOTOA HUDUMA KWA WANANCHI” DC MTATIRO
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amewataka Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutumia lugha nzuri wanapowahudumia wananchi.
Mhe. Mtatiro ameongea hayo leo tarehe 4 April, 2024 katika kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Manispaa ya Shinyanga kilichofanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya wa Shinyanga.
“ Niwaombe tumieni lugha nzuri mnapotoa huduma kwa wananchi kwani mnapotumia lugha nzuri katika kuwahudumia wananchi haitawapunzia taaluma yenu bali inawajengea uhusiano mzuri baina yenu na wananchi”. amesema Mhe. Mtatiro
Aidha, Mhe. Mtatiro amewataka wakuu hao kwenda kusimamia utatuzi wa kero za wananchi na kuzimaliza kwa wakati ili kuendelea kujenga uhusiano mzuri baina ya wananchi na watumishi.
Pamoja na mambo mengi Mhe. Mtatiro amewaagiza kwenda kusimamia vizuri miradi yote ya maendeleo kwa uadilifu na kukamilika kwa wakati, kusimamia vyanzo vya mapato na kuibua vyanzo vipya vya mapato vya muda mfupi na muda mrefu, kuendelea kufanya kazi za umma kwa kuzingati misingi na kunua za sheria ya kiutumishi, kuendelea kuhamasisha upandaji miti pamoja kuweka mikakati ya kukuza uzalishaji wa pamba kwa wingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa niaba ya Manejimenti ya Manispaa amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kuendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Manispaa na kumuhaidi kuendelea kushirikiana nae katika majukumu ya kazi mbalimbali kwa wakati wowote huku akikiri kupokea na kwenda kuyafanyia kazi maagizo yote aliyoyatoa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga