- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkuu wa mkoa wa shinyanga Mhe. Anamringi Macha amezitaka taasisi za Serikali, binafsi na wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga kuendelea kutetea haki za wanawake ili kuweka haki, usawa na ushirikishwaji katika sekta mbalimbali ili kuchochea maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.
Mhe. Macha ameyasema haya leo Machi 06, 2025 katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake kimkoa maadhimisho ambayo yamefanyika katika kata ya Bugarama Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
“Wanawake wakipata haki zao, wakiwezeshwa, wakishirikishwa ni moja ya kichocheo cha maendeleo katika jamii zetu, kwa sababu watafanya kazi zao za kipato bila kukandamizwa, ndiyo maana Mhe. Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani alileta kampeni hii ya msaada wa kisheria ili watu wote wapate haki na usawa bila kumuonea mtu yoyote kulingana na jinsia yake, ni mhimu sana taasisi za serikali, mashirika binafsi na wananchi kwa ujumla kuhakikisha wanawake hawa wanapata fursa sawa na wanaume”. Amesema RC Macha
Kwa upande wakea afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Bi.Rehema Edson amesema katika kutekeleza agizo la serikali Mkoa wa shinyanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi cha Tsh. 5,288,213,787 zimetengwa kwa ajili ya vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa kwa kila Halmashauri husika.
Katika hatua nyingine Bi. Rehema amesema kupitia kongamano lililofanyinka ndani ya siku za maadhimisho jumla ya mada nne zilifundishwa kwa wanawake ili kuwajengea uelewa juu ya malezi bora ya familia zao. MALEZI YA MAKUZI, UONGOZI,UWEZESHAJI NA AFYA YA AKILI.
Maadhimisho haya yalikuwa yakiambatana na Kaulimbiu isemayo; “WANAWAKE NA WASICHANA 2025: TUIMARISHE HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI” ambapo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Arusha Machi 08,2025.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga