- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga wametambulisha rasmi Programu ya TAKUKURU Rafiki ambayo inatajwa kuwa na mageuzi makubwa kwa wananchi na wadau ambao wataweza kishiriki katika kukabili tatizo la rushwa kwenye utoaji wa huduma kwa jamii na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akiwaeleza wajumbe waliohudhuria utambulisho huo, Mkuu wa Dawati la Uelimishaji kwa Umma TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bi. Helga Mfuruki alisema kuwa katika utekelezaji wa programu hiyo ambayo inaakisi maana halisi ya nejo "rafiki" ambapo itabeba dhana ya kuwa na karibu kwa ushirikiano na wananchi pamoja na wadau mbalimbali kwa kutumia vikao ambavyo vitaitishwa nankuendeshwa katika ngazi ya Kata zote.
Helga alifafanua zaidi kuwa, mikutano ya hadhara itakuwa moja kati ya njia bora kabisa ya kuisogelea jamii na kuishirikisha katika kuzitambua na kuziibua kero ambazo zipo kwenye utoaji au upokeaji wa huduma kama vile Afya, Elimu ikiwa ni pamoja na namna mchakato wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya ujenzi wa miundombinu au maji.
"Aidha utambuzi wa kero hizo ni muhimu sana kwani zikiachwa pasipo kutatuliwa au kupatiwa ufumbuzi zinaweza kupelekea kutokea kwa vitendo vya rushwa jambo ambalo Takukuru isingependa kuendelea kutokea hasa katika utoaji wa huduma za ya elimu, afya, nk", alisisitiza Helga.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Uzuiaji Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Ndg. Reuben Chongolo alisema kuwa katika vikao hivyo ambavyo vitahudhuriwa na wananchi, viongozi wa kisiasa, watendaji wa serikali na wazabuni mbalimbali watashirikiana kwa pamoja katika kuzitatua kero hizo au kuweka mipango mikakati ya utatuzi wake kwa kushirikiana na TAKUKURU wenyewe.
Kufanikiwa vema kwa programu hiyo kutakuwa na faida zaidi katika kukuza ustawi wa Utawala Bora, kutaweza kuzuia vitendo vya rushwa visitokee kabisa kwenye utoaji wa huduma kwa umma na katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha faida nyinginezo ni pamoja na kuokoa fedha za umma ambazo zitaweza kutumika katika kujengwa kwa miradi bora zaidi, endelevu na yenye kukidhi thamani ya fedha iliyotumika.
"Mwisho kabisa TAKUKURU inapenda kutoa wito kwenu viongozi, watumishi na wananchi wote kwa ujumla kuwa sasa imekuja karibu zaidi nanyi katika sura ya rafiki zaidi ili tushirikiane kuzuia vitendo vya rushwa visitokee katika utoaji wa huduma kwa umma na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia programu hii ya TAKUKURU Rafiki", alisema Chongolo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga