- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Geoffrey Mwangulumbi, leo asubuhi tarehe 23/06/2021 ameitisha kikao kifupi cha watumishi akiwatahadharisha juu ya wimbi la tatu la ugonjwa wa KORONA.
Alisema kwa sasa Taifa liko katika awamu ya tatu ya maambukizi ya virusi vya korona, hivyo tahadhari kubwa inatakiwa kuchukuliwa na kila mtu kuanzia ngazi ya familia mpaka kitaifa.
Aidha Mkurugenzi alisisitiza uvaaji wa barakoa pamoja na kunawa mikono kwa maji tiririka na kupaka SANITISER mara kwa mara unapokuwa ofisini na nje ya ofisi pamoja na kutofanya mikusanyiko isiyo ya lazima
Katika kutoa msisitizo huo, alisema tuwaelimishe watoto wetu majumbani pamoja na mashuleni kwani Awamu ya tatu ya maambukizi ya virusi vya KORONA ni hatari zaidi ya maambukizi ya awamu ya kwanza na ya pili na inawaathiri watoto tofauti na maambukizi ya awali ambapo watoto walikuwa salama.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga