- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Serikali mkoani Shinyanga imezidua Kampeni harakishi ya kuibua ugonjwa wa kifua kikuu kwa mkoa wa shinyanga inayokwenda sambamba na utoaji wa huduma na matibabu kwa wagonjwa watakaobainika na dalili na maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu.
kampeni hii imezinduliwa leo Februari 08, 2025 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, kampeni iliyofanyika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa shinyanga iliyopo manispaa ya shinyanga ambapo ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi na wakazi wote wa mkoa huu kujitokeza kupima na kupata huduma, ushauri, vipimo na matibabu yanatolewa bure kwa wananchi wote mkoani shinyanga.
“Bila afya hakuna maendeleo serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya kila liwezekanalo Kuhakikisha afya za wananchi zinakuwa njema, rai yangu kwa wakazi wa mkoa wa shinyanga tujitokeze kupima maambukizi ya kifua kikuu, na kutumia dawa ipasavyo kulingana na ushauri wa wataalamu wa ugonjwa huu”. Amesema Mhe. Macha.
Kwa upande wake mganga mkuu wa mkoa wa shinyanga Dkt.Yudas Ndungile amesema malengo ya mkoa ni kuwafikia takribani wananchi 1,349 ambapo mkoa wa shinyanga kitakwimu wanaishi na maambukizi ya kifua kikuu.
Naye Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani Hospital ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga ambae pia ni Mganga Mfawidhi wa Hosptali hiyo Dkt. John Ruzila amesema tafiti zinaonyesha 25% ya wakazi wanaishia na Maambukizi ya kifua kikuu ambapo kinaathiri kwa asilimia kubwa mapafu ambapo dalili zake ni kikohozi, homa za mara kwa mara, mwili kupungua uzito, kutokwa na jasho haswa nyakati za usiku.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga