- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameyataka mashirika kuendelea kuunga mkono na kushirikiana na serikali katika kuendelea kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Mhe. Macha ameyasema haya leo Oktoba 3,2024 wakati akizindua mradi wa jengo la choo chenye matundu kumi na mbili,kichomea taka Pamoja na chumba maalumu cha kubadilisha taulo za kike vilivyojengwa na shirika lisilo la Kiserikali la Flaviana Matata Foundation katika shule ya sekondari Masekelo,kata ya masekero Manispaa ya Shinyanga.
“Mazingira ya kujifunzia yakiwa safi hata wanafunzi watatulia shuleni, ndiyo maana serikali inaendelea kuweka mazingira bora kwa watoto wa kike ili waweze kujisitiri wakati wa masomo pindi wanapokuwa mazingira ya shuleni,niwaombe tu mashirika yasiyo ya kiserikali tuendelee kuweka mazingira rafiki kwa wanafunzi wa kike mashuleni”. amesema Mhe. Macha.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo Mwanzilishi wa shirika lisilo la kiserikali la Flaviana Matata Foundation Bi. Flaviana Matata amewasihi wazazi kuwawezesha Wanafunzi hao kutimiza ndoto zao kielimu kwa maslahi mapana ya taifa pamoja na kuendelea kuunga mkono serikali, kuweka mazingira rafiki kwa Watoto wa kike wakati wa masomo hususani wakati wa hedhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl.Alexius Kagunze ameshukuru jitihada zilizofanywa na shirika hili huku akisema Manispaa ya Shinyanga itaendelea kulinda miundombinu hiyo ili iweze kudumu Pamoja na kufanya ukarabari wa vyoo vya zamani ili wanafunzi wa kike waweze kupata ufaragha wakati wa hedhi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga