- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MNDEME AWATAMBELEA WAHANGA WALIOBOMOLEWA NYUMBA KUFUATIA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 5 Marchi, 2024 amewatembelea wahanga waliobomolewa nyumba kufuatia mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumamosi tarehe 2 Marchi, 2024 katika kijiji cha bugayambelele kata ya kizumbi akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa pamoja na kamati ya maafa ya Manispaa ya shinyanga ambapo nyumba 79 zimebomoka na kuezuliwa paa.
Akitoa salamu za pole kwa wananchi wa kata ya kizumbi kijiji cha bugayambelele Mhe. Mndeme amewataka wakazi wa bugayambelele kuendelea kuchukua taadhari ya kutoka katika makazi ambayo tayari yanaonesha si imara na kuwasahuri mvua zitakapo isha wajenge nyumba zenye uimara japo kwa kuweka misingi imara ili kuepuka maafa wakati wa mvua.
“ Poleni sana ndugu kwa kupoteza nyumba na baadhi ya mifugo jukumu la serikali ni kulinda watu na mali zao hivyo niwaombe pindi mvua zitakapo malizika tujitaidi kujenga nyumba zenye uimara angalau kwa kujenga misingi iliyoimara na kuezeka kwa ubora zaidi ili kuepuka maafa wakati wa mvua.” amesema Mhe. Mndeme
Pamoja na mambo mengine diwani wa kata ya kizumbi Mhe. Reuben Kitinya ameishukuru serikali kwa kuwa mstari wa mbele pindi wananchi wanapopata changamato kwa kutoa misaada mbalimbali na kuwapatia hifadhi za makazi ya muda pindi wanapokosa makazi ya kuishi.
Aidha, kufuatia mvua hii iliyonyesha jumla ya kaya 68 zenye watu 276 zimeathirika , idadi ya majeruhi 3 ambapo wamepatiwa matibabu na wanaendelea vizuri, nyumba 79 zimeathirika kwa kubomoka na kuizuliwa paa , makanisa 2 na msikiti 1 yamebomolewa na jumla ya kuku 314 wamekufa.
Kamati za maafa kwa kila kata zinaendelea kutoa elimu na tahadhari juu ya mvua hizi zinazoendelea kunyesha.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga