- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MNDEME AONGOZA KONGAMANO LA WANAWAKE WA MKOA WA SHINYANGA LA KUMPONGEZA MAMA SAMIA .
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 12 Oktoba, 2023 ameongoza kongamano la Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa anayofanya kwa Wanashinyanga katika ukumbi wa shule ya sekondari Savannah plain ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumzo katika kongamano hili Mhe. Mndeme amesema kwamba Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga wameua kumpongeza Rais wetu kwa sababu Shinyanga ya sasa sio Shinyanga ya zamani, maendeleo makubwa ya kiumchumi na kijamii yanaonekana, Wanashinyanga tunasema kila kijiji kimefikiwa hakuna kilichosimama kazi inaendelea kwa vitendo.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amegusa kila eneo mpaka vijijini, Wanashinyanga tunasema kila vijiji vimefikiwa hakuna kilichosimama kazi inaendelea kwa vitendo " alisema Mhe. Mndeme
Sanjali na hilo Mhe. Mndeme ameeleza kuwa kwa kipindi cha awamu ya sita Mkoa wa Shinyanga umepokea fedha takribani Tsh Trioni 1 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Miradi ya Maendeleo kupitia Mamlaka ya Serikali za Mitaa , Serikali kuu pamoja na Taasisi za Serikali katika Sekta ya Elimu, Afya, Maji, Kilimo,Nishati, Utawala, Viwanda na Uwekezaji pamoja na Sekta ya madini,
Aidha, Mhe. Mndeme ameeleza kuwa Mhe. Rais ametoa jumla ya bilioni 30.61 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kunusuru kaya masikini kwa kuboresha nyumba zao za kuishi pamoja na kuwaanzishia miradi ya kujiongezea kipato ikiwemo ufugaji, kilimo na ujasiriamali.
Pamoja na mambo mengine Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga wanamshukuru sana Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapenda na kuwaletea maendeleo makubwa Wanashinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga