- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MNDEME AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA SOKO KUU MANISPAA YA SHINYANGA
Na. Shinyanga MC
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 11 Septemba, 2023 amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa soko kuu, huku akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Viongozi mbalimbali toka Serikalini pamoja na watumishi kutoka Manispaa.
Katika ziara hiyo Mhe. Mndeme aliweza kukagua ujenzi wa soko kuu hilo wenye jumla ya vyumba 106 ambapo vyumba 41 vipo katika hatua ya ukamilishaji kwa kuwekea mifumo ya umeme na vyumba 67 vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
"Nimekagua ujenzi wa soko hili kasi ni ndogo sana hivyo naomba kasi iongezeke ili wafanyabishara wetu wawezi kuanza biashara na kwa upande wa Manispaa waanze kukusanya mapato ya ndani "alisema Mhe. Mndeme
Aidha, Mhe. Mndeme pia ameagiza ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga kutoa tangazo la wazi linaloonesha gharama za upangishaji wa vyumba vya soko hilo ili kuepusha usumbufu wowote utakaojitokeza huku akiwasii ugawaji wa vyumba katika soko hilo uwe wa kushirikisha wafanyabiashara na kila anayestahili kupewa chumba apatiwe, pia ujenzi uwo ujengwe kwa ubora kwa kuzingatia bajeti iliyopangwa pamoja na kuagiza kila soko kujenga chumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea watoto.
Sanjali na hilo Mhe. Mndeme amewataka wafanyabiashara wa soko hilo kufanya biashara za halali huku akiwata kufanya biashara kwa kufungua mapema na kufunga kwa kuchelewa ili kuongeza zaidi mzunguko wa fedha.
Soko kuu la Manispaa ya Shinyanga linajengwa kwa kutumia mapato ya ndani ya Manispaa na gharama zitakazo tumika mpaka kukamilika kwa ujenzi uwo ni kiasi cha Tsh bilioni 1,840,000,000/=
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga