- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MNDEME AFANYA KIKAO KAZI NA MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 10 Oktoba, 2023 amefanya kikao kazi na Maafisa Tarafa na Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa wa Mkoa wa Shinyanga katika shule ya sekondari Savanna iliyopo kata ya ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika kikao kazi Mhe. Mndeme amewapongeza viongozi hao kwa kusimamie vizuri majukumu yao ya kazi ikiwemo miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yao ya kazi.
"Niwapongeze kwa ujumla kwa usimamizi mzuri katika majukumu yenu ya kila siku ikiwemo usimamiaji wa miradi ya maendeleo mnayosimamia katika maeneo yenu hongereni sana" alisema Mhe. Mndeme
Aidha, Mhe. Mndeme amewaeleza viongozi hao kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya maendeleo makubwa katika kata, mitaa na vijiji hivyo ni jukumu lenu kuendelea kusimamia maendeleo hayo kwa ukaribu ili tuendelee kupokea fursa mbalimbali katika maeneo yenu.
Sanjali na hilo, Mhe. Mndeme pia awewataka viongozi hao kutumia lugha nzuri pale wanapowahudumia wananchi pamoja na kuacha kutumia simu zisizo za lazima wakati wanapowahudumia wanachi.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mndeme ametoa maagizo kwa viongozi hao ili waweze kusimamia mambo mabalimbali katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kutoa taarifa kwa wananchi pindi fedha za miradi zinapowasili.
Pia akawataka kwenda kutatua kero za wananchi, kusimamia utunzaji wa mazingira, kutoa taarifa kwa mtu yeyote atakaye fanya ukatili ikiwemo ndoa za utotoni, ulinzi na usalama pamoja na kutoa tahadhari ya mvua ya el nino kwa wananchi hasa wanaokaa maeneo ya mabondeni kuanza kuhama.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga