- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, Shinyanga Manispaa
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Sophia Mjema, amewataka wananchi walio ndani ya mkoa wake kupanda miti kwa wingi katika maeneo yanayowazunguka, ili kukuza ustawi mzuri wa mazingira na kuondoa athari za ukame.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mh. Sophia Mjema, akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Butengwa.
Mjema ameyasema hayo leo Novemba 26, 2022 wakati wa uzinduzi wa msimu wa upandaji miti, uliofanyika katika Shule ya Sekondari Butengwa iliyo Kata ya Ndembezi, ambapo aliongoza Taasisi mbalimbali zilizojitokeza, kupanda jumla ya miti 500 na mingine 500 wakipewa wananchi.
Mh. Sophia Mjema (wa pili kushoto) akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza D. Tumbo (wa kwanza kushoto), pia MKuu wa Wilaya ya Shinyanga, Mh, Jasinta Mboneko pamoja na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, John Tesha, ambao wote walishiriki zoezi la upandaji miti.
Katika uzinduzi huo, Mjema ametoa kauli hiyo akisisitiza kuwa ili mazingira yawe mazuri na kuchochea maendeleo ya ustawi mzuri wa mazao na hata maji, ni lazima kuwe na miti mizuri ambayo itasaidia kutunza mazingira.
“Tumezindua shughuli ambayo itaenda kufanyika kwenye Halmashauri zote, tuhamasike tupande miti kwa wingi, hii itatusaidia kutengeneza mazingira bora ya kuishi.
“Miti inasaidia udongo kuwa na rutuba nzuri pamoja na uzalishaji mzuri wa maji. Tusipofanya haya tutakosa maji, ukame utakuja na tutakosa chakula. Lazima tuzingatie haya na nguvu kazi ya kupanda miti hususani ya matunda lazima iwekezwe,” amesema Mjema.
Wadau kutoka taasisi mbalimbali waliojitokeza Shule ya Sekondari Butengwa kushiriki zoezi la upandaji miti wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Sophia Mjema.
Katika hatua nyingine, Mh. Mjema ametoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya na Halmashauri zote katika Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha elimu ya upandaji miti inatolewa, sambamba na kutenga maeneo maalum kwa ajili ya vitalu vya miti na misitu.
Aidha, Mjema amesema lengo la idadi ya mkoa kupanda miti ni milioni 9, lakini mpaka sasa iliyofikiwa ni milioni 8.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga