- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
RC MACHA AZINDUA KAMPENI YA UTOAJI CHANJO SARATANI YA MLANGO WA SHINGO YA KIZAZI “HPV” KWA WASICHANA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, amezindua Rasmi kampeni ya utoaji Chanjo ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi (HPV) kwa wasichana,huku akitoa onyo kwa atakae bainika kufanya upotoshaji juu ya Chanjo hiyo Serikali itamchukulia hatua.
Uzinduzi wa utoaji wa Chanjo hiyo HPV umefanyika leo Aprili 22, 2024 katika Shule ya Msingi Ndala “A” Manispaa ya Shinyanga ambayo itawafikia Wasichana 198,865 wenye umri wa kuanzia miaka 9-14 ili kuwakinga dhidi ya Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi.
akizungumza kwenye uzinduzi huo Mhe. Macha ametoa wito kwa wazazi kuwaruhusu Watoto wao wapatiwe Chanjo hiyo ya (HPV) ili kuwakinga dhidi ya Ugonjwa wa Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi, huku akiwaonya wale ambao watapotosha juu ya Chanjo hiyo Serikali itawachukulia hatua kali za kisheria.
“Chanjo hii ya Saratani ya Mlango wa Shingo ya kizazi ni salama kabisa na haina madhara yoyote, na ilianza kutolewa tangu mwaka 2014, na tangu kipindi hicho hakuna madhara yoyote ambayo yametokea, sasa kwa wale ambao wataanza upotoshaji Serikali itawachukulia hatua.”amesema Mhe. Macha
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungulile, amesema tayari Chanjo zote zipo kwenye Vituo, ambapo zitatolewa katika maeneo ya Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na kwenye Vituo vya Afya, na watawafikia wasichana 198,865 wenye umri wa kuanzia miaka 9-14 na watapewa Dozi Moja tu.
Chanjo hii imeanza rasmi leo Tarehe 22 Aprili na kumalizika 28 Aprili, 2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga